Chapisho Jipya

Njia za uhakika za kujiingizia kipato kwa blog

KARIBU SANA MSOMAJI hebu ungana nami

1.KUWEKA HABARI NA TAARIFA MBALAMBALI.
Unaweza kutumia blog yako kuweka au kutangaza habari mbalimbali za kikanda,kitaifa au hata za kimataifa.Habari kwa maandishi,Habari kwa Picha na Habari kwa Sauti na Habari kwa Video,Chaguo ni lako.
2.KUWEKA TAARIFA ZAKO BINAFSI
Unaweza kutumia BLOG kutunzia taarifa zako mbalambali kama vile matukia\o yako ya kila siku,taarifa zako za nyumbani n.k ANGALIZO:KAMA UNATAKA UWEKE TAARIFA ZA SIRI IWEKE BLOG YAKO KATIKA PRIVATE,Baada ya kufanya hivyo hakuna mtu yeyote atakayeweza kuona taarifa zako hata kama akaingia katika BLOG YAKO.
3.Kutangaza biashara yako
NDIO, Kama una biashara yako na unataka kuinadi kupitia blog basi inawezekana kabisa hapa kuna mbinu zinazohitajika ili uweze kufanikiwa katika hili.Lugha ya Mvuto,Utumiaji mzuri wa Picha,kuwa Mbunifu na jifunze jinsi ya kuongea na wateja.Toa ofa na mengineyo.
4.KUTUMIA BLOG KWA AJILI YA MAWASILIANO KATIKA KAMPUNI
Kivipi, unaweza kuitumia blog yako kwa ajili ya mawasiliano ya kampuni au Shirika mara nyingi blog za aina hii huwa zinwekewa password hivyo Mtu asiyehusika hawezi kuingia.Hata wewe unaweza kufanya pia.
5.Kutumia Blog katika Taasisi Mbalimbali
Unaweza pia Kuitumia Blog katika taasisi mbalimbali kama vile Shule,Vyuo,Taasisi za kidini na hata Vikundi mbalimbali.Blog itasaidia kurahisisha Mawasiliano.Kwa mfano Blog ya Shule inaweza KUTUMIKA kuweka taarifa mbalimbali na matukio ya Shule/Chuo kama vile Ratiba ya Vikao,Ratiba za Mitihani na mengineyo.Blog ya shule na Chuo pia inaweza kutumika kuweka JOINING INSTRUCTIONS(Hii ni barua inayotoa mwongozo wa MAELEKEZO Y KUJIUNGA NA CHUO AU SHULE HUSIKA) Kumekuwa na ugumu wa kupatikana kwa barua hizi na hivyo kuwafanya wanafunzi MUDA MWINGINE, kusafiri umbali mrefu kwenda shuleChuo kuchukua JOINING INSTRUCTIONS LETTER,BLOG INAMALIZA TATIZO HILI.

TUNAKUTENGENEZEA BLOG KWA GHARAMA NAFUU KUANZIA TZS 20,000/= na website 35000(pamoja na domain name ya .xyz)TU.
TUPIGIE 



ZIFUATAZO NI NJIA AMBAZO UNAWEZA KUZITUMIA KUJIINGIZIA KIPATO KWA KUPITIA BLOG.

Hii ni sehemu muhimu ambayo karibu kila anayefungua blog anataka afahamu jinsi gani anaweza kuingiza kipato kwa kupitia blog.Swali linakuja je ni kweli mtu unaweza ukaingiza fedha kwa kupitia blog? Jibu ni NDIO unaweza kuingiza kipato kwa kupitia blog.Kabla ya yote unatakiwa ufahamu kuwa fedha ni thamani na thamani yoyote haipatikani pasipo kuifanyia kazi,hivyo kuingiza fedha kupitia blog vivo hivyo inahitaji ujitoe kwa kweli.Fahamu pia kuwa inahitaji muda hadi uweze kuingiza kipato kupitia blog.Urefu wa muda unatofautiana kuna ambao wanaanza kjiingizia kipato ndani ya siku kadhaa wengine miezi kadhaa na wengine inafikia hadi mwaka au zaidi.Yote haya hutegemea Aina ya BLOG na makala zinazowekwa,Kwa mfano ni vigumu kuingiza fedha haraka kama utafungua blog ya ktoa taarifa na habari.Hata hivyo ukiwa Mbunifu zaidi hakutakuwa na kikwazo.


1.KUWEKA MATANGAZO YA WATU KISHA WAKAKULIPA
Hii ni njia namba moja na maarufu sana utakayoweza kuitumia kujiingizia kipato kupitia blog yako.Fahamu kuwa kuna wafanyabiashara ambao wanatafuta wateja mtandaoni.Ili uweze kumshawishi mtu aweke tangazo lake katika blog yako lazima blog yako iwe na vitu vifuatavyo:
i)Lazima blog yako iwe na watembeleaji wengi.
i)Lazima blog yako iwe hai(hii ina maana ya kwamba blog yako iwe inawekwa makala mara kwa mara,isiwe umeweka makala leo,kisha unakaa mwezi mzima haujaweka makala).
2.Kuifanya blog yako iwe ya kulipia
Hii ni njia ya pili unayoweza kuitumia kujiingizia kipato kupitia.Faida kubwa iliyopo ni kwamba wewe ndiye unaamua nani atazame blog yako.Unaweza ukaifunga blog yako na ikawa hakuna mtu anayeweza kuingia katika blog yako bila ya wewe kumruhusu.Na utamruhusu pale atakapofanya malipo.
KUMBUKA:Ili kuweza kutumia njia hii na uweze kufanikiwa katika kujiingizia kipato kupitia blog yako ni lazima uandike vitu vya thamani,yaani uandike vitu ambavyo vina faida kwa watu,pia viwe vitu ambavyo havipatikani sehemu nyingine yoyote bure.Usihofu sio kazi kubwa unachotakiwa kufanya ni kujifunza sifa au stadi za blogger aliyebobea.
Blogger=Mtu anayemiliki blog au anayeandika makala katika blog au mwendeshaji wa blog.
Jifunze jinsi ya kuwa Blogger aliyebobea(Mtaalamu).
Zifuatazo ni sifa za Blogger aliyebobea(Unatakiwa uwe nazo sifa hizi ili uweze kujiingizia kipato kupitia Blog).Usijali sio lazima zote,Anza na chache Nyingine Utajifunza Baadae.
i/.Uwezo wa kuandika makala zenye mvuto na zinazoeleweka.
ii/.Uwezo wa kufanya tafiti,Blogger anatakiwa awe na uwezo wa kufanya utafiti juu ya yale anayotaka kuandika.
iii/.Blogger anatakiwa awe na uzoefu na Mitandao tafutaji(Search Engines) .
.Blogger anatakiwa awe na ujuzi wa kuandika kiufasaha.Andika kitu kinachoeleweka.
iv/.Kuwa na Nidhamu katika Blog yako.Weka Makala lkatika blog yako kwa Utaratibu Maalumu.
v/.Ujuzi katika matumizi sahihi ya picha namichoro.Picha na michoro ina umuhimu Mkubwa katika ka kuonngeza mvuto wa Makala.
.
3.Kuweka matangazo ya Google ADsense/Adword.
Unaweza kuweka Matangazo kutoka Google /Wordpress na Ukalipwa kutokana na idadi ya watembeleaji wa blog yako mfano amazing fact 360 watakaotembelea Blog hiyo.Kuna sifa za kuweza kuruhusiwa kuweka Matangazo ya Google au WordPress.
pia unaweza kuweka matangazo ya YLLIX ambayo ndiyo mbadala mkubwa wa adsnse kwa waandishi wapya soma zaidi hapa kuhusu yllix
Monetize your website traffic with yX Media
Hii pia inahitaji blog yako iwe na makala za kutosha na iwe na watembeleaji wakutosha.

4.Kutoa kozi mbalimbali ambazo watu watakuwa tayari kujiunga na kozi hizo NA KUZISOMA KWA MALIPO UTAKAYOWATOZA.Hii wala si kazi kubwa ingawa inahitaji muda na kujitoa.Kama una ujuzi wowote na unataka kuwafikishia watu kisha wakulipe basi fahamu kuwa kupitia blog unaweza kuwafikia watu wengi sana utaifanikisha kazi hii kupitia blog yako.Nakushauri kutumia Kiswahili kwani ndiyo lugha ambayo watanzania wengi wana umahiri nayo kuliko lugha nyingine.
Ili uweze kufanikisha hili unatakiwa uweke ulinzi(wa password) KATIKA KOZI ZAKO.


5.Kutangaza biashara zako.
Tukiacha kutangaza biashara za watu pia wewe mwenyewe unaweza kutangaza biashara zako na ukaongeza wateja kupitia blog yako.Hii inajumuisha bidhaa zote za mtandaoni na zisizo za mtandaoni.Unaweza kuandika vitabu mbalimbali kuanzia vya masomo hadi vya hadithi na kadhalika.Vitabu hivi utaviandika kupitia MS Word au program nyingine inayoweza kufanya huduma hiyo na utawauzia wateja kwa kuwatumia katika email zao.



Ili uweze kupata soko la uaminifu unaweza ukaandika kitabu cha kwanza na kukitoa BURE KABISA au kwa Ofa.Usishangae, kufanya hivi kutajenga uaminifu mkubwa na kama kitabu chako kitakuwa kizuri basi unaweza kupata soko kubwa kwa vitabu utakavyovitunga baadae na kuviuza.

KUONGEZA WATEMBELEAJI KATIKA BLOG YAKO
  • Itangaze Blog yako katika Mitandao ya kijamii,kama vile Facebook,Twitter,Instagram,WhatsApp na kadhalika.
  • Andika makala zenye mvuto na zinazoeleweka.Hii itawafanya watembeleaji wawe wanatembelea mara kwa mara.
  • Itangaze blog yako kwenye mitandao mikubwa yenye watembeleaji wengi.
  • Kuwa na utaratibu wa kukomment katika mitandao mikubwa yenye watembeleaji wengi.kisha acha link ya blog yako,kwa njia hii unaweza kupata watembeleaji,ila jitahidi kukomment kitu chenye maana/thamani.
  • Chukua maoni ya wasomaji wako na uyafanyie kazi,hii itawafanya wasomaji wako waendelee kutembelea blog yako kwani watakuwa wanakipata wanachokitaka.Ukienda kinyume na wasomaji wako ,wanaweza kukukimbia na kutafuta blog nyingine itakayowafaa.
  • Weka makala katika blog yako kwa utaratibu maalumu.
  • Andika makala za muda mrefu.Makala za muda mrefu zina manufaa makubwa kwani hatakama makala uliiandika mwaka uliopita bado itakuwa na thamani.Na watu wataendelea kuisoma kwani bado ujumbe unatumika.Makala za habari zinadumu kwa muda mfupi sana.
  • Kuwa mbunifu ifanye blog yako iwe ya kuvutia,Buni Mwonekano wa blog yako uwe wa kuvutia,kuna rangi nyingine Ukiweka unafukuza watembeleaji(Color Psychology).
  • Kichwa cha makala kinachovutia.
  • Jitahidi kuandika kighwa cha makala kinachovutia ili umshawishi MSOMAJI Kuendelea kusoma.
  • Watambue wasomaji wa Blog yako.

Ni vema uwe na wasomaji 10 wa blog yako unaowatambua,kuliko kuwa na wasomaji 100 usiowatambua.
Ninapozungumzia kufanikiwa kupitia BLOG yako wengi wanweza wakapeleka mawazo yao katika UCHUMI,HASHA sina maaan hiyo,bali ninachikusudia hapa ni jinsi gani unaweza kufanikiwa katika blog yako.Hii ni kwa sababu watu walio wengi hawadumu katika blog zao ,yaani mtu akifungua blog baada ya muda mfupi tu miezi kadhaa(na wengine hata siku kadhaa) HIVYO mtu wa aina hii ameshindwa kufanikiwa katika blog yake.
Zifuatzo ni sababu zinazowafanya Watu wengi washindwe kufanikiwa kupitia blog zao.

1.Kiwewe cha BLOG.
Nini maana ya kiwewe cha blog? Kiwewe cha Blog ni hali ya mtu kutamani sana awe na(amiliki) blog,na kufikiria kuwa ni kazi rahisi sana,Ukweli ni kwamba KUTENGENEZA BLOG ni kazi rahisi sana,tatizo linakuja katika jinsi ya kuiendesha.Inahitaji nidhamu ya hali ya juu sana la sivyo safari yako ya blog itaishia njiani.Sababu hii huwafanya wengi waachilie mbali kuhusu blog na hivyo kushindwa kufikia malengo.

2.UTIAJI Chumvi wa baadhi ya watu katika Matangazo yaao ya kujinadi.
Kuna baadhi ya watu wanatia chumvi sana kiasi kwamba inaonekana kuwa kutengeneza/kujiingizia fedha kupitia blog ni kama kazi ya saa moja tu.Mfano unaweza ukakuta tangazo linalosomeka ‘’FUNGUA BLOG LEO UANZE KUPOKEA FEDHA’’ au “FUNGUA BLOG LEO UANZE KUINGIZA KIPATO CHA MAANA,SI AJABU WENGINE WANAFIKIA HATA KUSEMA UWE TAJIRI’’.Matangazo ya namna hii na kwa mtu mwenye uelewa wa chini anayachukulia kama yalivyo.Pia wanashindwa kufahamu kuwa hiyo ni Lugha ya kibiashara tu.SI UONGO BLOG inaweza kukufikisha KWENYE UTAJIRI Lakini si kwa haraka na kiurahisi namna hiyo.Watu wa namna hii mara nyingi huishia kufunguia blog tu na kuiacha kwani anakuta mambo tofauti na vile alivyoambiwa.

3.KUKOSA CHA KUANDIKA
Wapo wanaoshindwa kupata cha Kuandika,na hivyo huishia kati katika safari yao ya Blog.
>>>SULUHISHO:Hakuna kitu kipya Duniani usiogope kuona hakuna kipya,utakachoandika kwa kuona kila kitu kimeshaandikwa.Andika tofauti na Wenzako,kuwa Mbunifu na hii ndio faida ya kufanya utafiti kwani utafahamu mapungufu ya wengine katika makala zao na utajua jinsi gani utayarekebisha kupitia makala zako mpya utakazoandika.
PIA,Jijengee utaratibu wa kujisomea Soma Vitu Mbalimbali vitakavyokuongezea Maarifa.Soma mtandaoni,soma vitabu,soma magazeti n.k.Ukijijengea utaratibu wa kujisomea utaongeza maarifa ya kutosha yatakayokuwezesha kupata makala za kuandika,sio kucopy.
4.KUTOKUWA WAVUMILIVU


Kuifanya Blog yako iwe chanzo cha mapato inahitaji Muda wa kutosha.Sio rahisi kuanza kufungua Blog leo na kesho ukaanza kupokea fedha.Kutokana na hali hii watu wasiokuwa wavumilivu huamua kuachana na Blog.
>>>SULUHISHO:Inahitaji kuwa Mvumilivu ili uweze kufanikiwa katika blog yako.Kuwa Mvumilivu na tumia mbinu mbalimbali kuiboresha blog yako.

5.KUTOPATA WATEMBELEAJI
Kupata Watembeleaji katika Blog yako inategemea vitu vingi.Kuna watu wanapofungua blog na kuona hakuna watembeleaji huamua kuachana na blog.

1 comment:

  1. Je kuna madhara ya pale unapocopy na kupaste from one web to another web

    ReplyDelete