Chapisho Jipya

Kufanya Biashara katika Intaneti: Biashara 5 za Kuanza Nazo Bure

biashara-katika-intaneti-0
Wajasiriamali wengi wamekuwa wakitafuta mbinu mbalimbali za kufanya biashara aidha kwa kuuza huduma au bidhaa. Lakini wachache sana hasa Afrika ambao wanafikiria kufanya biashara katika intaneti. Kuna mbinu nyingi tofauti za kufanya biashara katika intaneti ambazo zinatoa fursa kwa wajasiriamali kujiongezea kipato.
Kinachohitajika ni simu au kompyuta yenye kuunganishwa na mtandao wa intaneti na pia kuwa umejiunga na mitandao ya kijamii ,au mmiliki wa tovuti au blogu (ambazo unaweza kupata bure) au barua pepe.
Zifuatazo ni baadhi ya programu zinazokuwezesha kupata fedha kupitia intaneti:

1. Kuuza Bidhaa za Biashara Yako Kupitia Tovuti 

Unaonesha biadhaa zako na bei,wanunuaji wanaziona na kuweka oda ya manunuzi. Wanalipa kwa Kadi ya Benki Credit /Debit Card) na fedha inaingia katika akaunti yako benki. Au kwa kutumia malipo kwa mfumo wa simu kama M-Pesa ,Tigo Pesa na Airtel Money kwa Tanzania.

2. Kuuza bidhaa za biashara ya watu wengine kupitia tovuti

Unajisajili na baadhi ya makampuni yanayouza bidhaa mtandaoni duniani kama Amazon na eBay na kisha kuonesha bidhaa zao katika tovuti au blogu au katika mitandao ya kijamii kama facebook na twitter. kisha watu wakinunua bidhaa hizi kupitia matangazo yako basi unapata kiasi cha malipo waliyofanya yaani kamisheni.
Kujiunga fuata linki:

 3. Kuuza Matangazo Kupitia Tovuti au Blogu

Kuna makampuni mbalimbali dunia ambayo yana wakutanisha watangazaji na wauzaji kupitia matangazo katika tovuti au blogu.
Watangazaji wanajiunga nakutuma matangazo ya biashara yao na wauzaji wenye tovuti wanajiunga nakuruhusu matangazo kuonekana katika tovuti zao.
Wauzaji wa matangazo wanalipwa kila tangazo linapoonekana katika tovuti au watu wanapo bonyeza matangazo haya.
Mfano ni adsense ,YLLIXchitika BuySellAds nk.
Unahitaji kuwa na tovuti au blog ili kufanikiwa katika programu hii.

4. Kufanya Kazi za Ajira Kupitia Mtandao

Kuna makampuni ambayo yanataka wafanyakazi katika mtandao ambao wanaweza kufanya kazi fulani na wanalipwa wakikamilisha.
Baadhi ya kazi ni kama kutengeneza tovuti, kutengeneza programu za komputa au simu, kuchapa,kusikiliza na kutohoa suuti kwenda maandishi n.k
Badhi ya mitandao inyotoa huduma hizi ni  surveycompare.net , odesk.comonlinejobs.net ,elance.com , peopleperhour.com na  fiverr.com

5. Kutangaza Biashara kwa Kutuma Linki

Mbinu hii ndiyo hasa ninayopenda kuisisitiza hapa. Sababu ya kusisitiza nimkwasababu inafanya kazi kwa haraka na urahisi. Huhitaji kuwa na tovuti wala blogu kufanikisha. Kama tu upo katika mitandao ya kijamii kama facebook,twitter,intagram na mingine kama skype,whatsapp na pia kwa email unaweza kufanikiwa sana kwa kutuma linki ambayo marafiki zako wakiifungua utapata malipo.
Mfano Nimesoma katika intaneti kitu kizuri juu ya kupunguza unene na nataka marafiki zangu wanene wafidike kama haupo katika bishara hii nitatuma linki katika kundi katika facebook mfano na sitapata chochote.
Lakini ukiwa katika programu hizi unawezeshwa wewe kupata malipo kila unapofanya hivyo. Rahisi
Kama una marafiki wengi basi uwezo wako wa kufanikiwa ni mkubwa sana
Ifuatayo ni mitandao inayotoa huduma hii:

i. paid2refer

Kampuni hili linakutaka ujiunge kisha shirikisha marafiki zako kwa kuweka linki katika mitandao ya kijamii,tovuti ,blogu na barua pepe. Kila mtu atakayefuata linki unapata $0.5 sawa na Tsh. 800/-
Na ukijiunga tu unapata $2 kwenye akaunti yako. Wanalipa kupitia MoneyGram na PayPal
Kujiunga: Bonyeza Hapa

ii. CashFly

Ukitaka kushirikisha marafiki linki yoyote nzuri katika mtandao basi unakopi hiyo linki kisha unaingia katika tovuti yao na kuifupisha. Baada ya hapo utakopi linki iliyofupishwa na kuishirikisha kwa marafiki katika mitandao ya jamii na tovuti au barua pepe. Kila mtu anayefuta lini unapata malipo
Marafiki wanapata habari nzuri na wewe unapata fedha
Jiunge hapa: Bonyeza Hapa

iii. adfly

Kama ilivyo CashFly;adfly wanakuwezesha kufupishalink na kusambaza kwa marafiki
Kujiunga: Bonyeza Hapa

iv. richlink

Kama ilivyo CashFly na adfly wanakuwezesha kufupishalink na kusambaza kwa marafiki
Kujiunga: Bonyeza Hapa

 v. PaidToClick

Programu hii ni tofauti na hapo juu. Hapa unajiunga kisha unapewa linki kadhaa za kuzifuata.
Unalipwa kwa kubonyeza linki na kusoma kila kliki inaweza ikakupa $2 sawa na Tsh. 3,500 hivi.
Kujiunga: Bonyeza Hapa

Anza Sasa

Shiriki na marafiki zako upate fedha. Mtandao wa intaneti umeleta fursa nyingi sana kwa kila mtu.
Unaweza ukaanza na programu mojawapo ili kupata uzoefu na kadiri unavyoendelea unaweza ukajaribu na nyingine.
Unaweza ukaanzisha blogu yako pia. Nirahisi  jaribu blogspot.com au wordpress.com

Unataka Blogu?

Unaweza ukawasiliana naSI  TUKUSHAURI NJIA NZURI NA MADA ZINZOWEZA KULETA WATEMBELEAJI WENGI

No comments