Chapisho Jipya

Makosa 5 Wanayoyafanya Wamiliki Wa Website Na Jinsi Ya Kuyaepuka

Katika dunia ya leo, kuwa na website ya kampuni au biashara si kitu cha anasa na pia si kitu cha hiyari bali ni cha lazima kwa kila mfanya biashara makini.
Maendeleo ya tehama yamefanya bei na gharama za kutengeneza na kumili website kushuka huku watengenezaji wa website hizi wakiwa karibu kabisa na mteja, leo hii unaweza kupata makampuni ya kutengeneza website kila kwenye kila kona ya mji. Sio hivyo tu, siku hizi kuna makampuni mengi ya Tehama yamekuwa yakiwawezesha watumiaji wake kuwa na website au blog bila gharama yoyote, mfano wake ni Wordpress na Blogspot.
 Kumiliki Website sio mwisho wa safari ya kibiashara, kwani unatakiwa kuifanya website yako iwe inayofanya kazi. Usiiche ilale usingizi mnono huku wewe ukiwa mmiliki wake unashindwa kuiamsha. Website inatakiwa kufanya kazi, iwe kama sehemu ya kuleta wateja (mfano saluni au hoteli), iwe kama sehemu ya biashara na mauzo(mfano wale wanaouza vitu online)na pia iwe sehemu ya kuwasiliana na wateja wako.
Wengi wamekuwa wakishindwa kufikia matokeo haya, ama kwa kutofahamu au kushindwa kujua fursa ambazo wanaweza kuzitumia. Hivyo leo hii tuangalie makosa ambayo wamiliki wengi wamekuwa wakiyafanya na jinsi ya kuyaepuka au kuyatatua.


Kukosa uelekeo.

Kama tulivyoona hapo juu, website sasa ni sehemu ya biashara, lakini wamiliki wengi wa website wa Tanzania hawajui nini wanaweza kufanya kwa kutumia website. Wengi huishia kwenye hatua ya kuwa na website. Tumewahi kufanya kazi na wafanyabiashara wengi, na wengi wao hupotea punde tu wanapokamilisha utengenezaji wa Website. Swali ambalo unatakiwa kujiuliza ni kuwa, Je nini lengo lako la kuwa na website?  Kuonesha kazi zako au kufanya biashara? Au kuwa na website ili na wewe uonekane una website?
Ili uweze kufanikiwa na kukufanya uone matunda ya website, unatakiwa ujue lengo na uelekeo wa website yako. Uelekeo huu ni lazima uendane na uelekeo wa biashara yako. Ukiwa kama mmiliki wa biashara, na kwa kushirikiana na mtu aliyekutengenezea website ambaye pia anafahamu jinsi ya kufungamanisha (align) biashara na tehama, muhakikishe website inakuwa sehemu ya biashara. Epuka wale waliojikita kwenye Tehama kwa Tehama bila kuangalia masilahi ya kibiashara kwani hilo sio lengo lako la kuwa na Website.

Kutotumia takwimu.

unatakiwa ujue takwimu za kiasharaTakwimu ni moja ya vitu muhimu kwenye website yoyote, lakini ni wafanyabiashara / wamiliki wachache mno ambao hata wanafahamu uwepo wake, usiongelee kuitumia. Ukweli ni kuwa, kama haujui watembeleaji wa website yako wanafika vipi, 
wanafanya nini, wanapenda kutembelea kurasa zipi nk, je utaweza vipi kupima uwezo wa website yako?
Takwimu hizi huweza pia kukupa picha halisi juu ya jinsi gani watu wanavyotafuta taarifa online, iwe ni kutafuta bidhaa, habari au hata anuani ya kwenda sehemu fulani. Hivyo kwa kutumia takwimu hizi, utaweza kupata picha halisi juu ya tabia za watembeleaji wa website yako. Utaweza kujua ni muda gani au kurasa zipi ndizo zinapendwa na watembeleaji bila kusahau kujua ni toka mji gani watembeleaji wanakuja kwenye website yako.
Chukulia mfano, wewe ni mmiliki wa website ya mgahawa ulio Arusha halafu kwenye website yako watembeleaji zaidi ya asilimia tisini wanatoka Dar, hii inamaana ufanisi kwa biashara yako unaweza usiwe mkubwa, ingawa nayo inategemeana na aina ya biashara.
Ili kutatua tatizo hili, tumia programu za takwimu, huku ukitafuta wataalamu ambao wanaweza kukutafsiria maana ya hizi takwimu kwenye lugha ya kibiashara zaidi.

Leo hii ukienda kwenye website nyingi utaona wameweka takwimu inayoonesha idadi ya watembeleaji, hii haina mchango mkubwa kwani kuna mambo mengi yanayotakiwa kuchimbwa kwenye kila takwimu ili kuweza kufungamanisha biashara na uwezekaji wa kwenye tehama.


Hakuna sehemu ya kutafuta taarifa (Search Botton)

Kwa website kubwa ambazo zina vitu vingi au kufanyiwa mabadiliko kila mara, sehemu ya kutafuta (search button) ni lazima, sehemu hii sio tu itasaidia kuokoa muda wa watembeleaji wa website ambao hawana muda wa kuanza kujaribu kurasa moja hadi nyingine, bali pia utasaidia kuongeza muingiliano kati ya website na watembeleaji.
Hivyo basi, hakikisha unakuwa na sehemu ya kutafuta taarifa kwenye website yako. Pia hakikisha unaungannisa kitafuto hiki na mitambo ya takwimu ili kukupa picha halisi ya ni vitu gani ambavyo watu wanavitafuta sana kwenye website yako. Chukulia mfano, wewe ni mmiliki wa saluni ya kinamama, endapo utakuwa na sehemu ya kutafuta na takwimu za utafutaji zinaonesha kuwa watu wengi wanatafuta weaving, hivyo basi utaweza kujua ni bidhaa gani watembeleaji wengi wanahitaji na kuweza kuingiza kama sehemu ya mpango wa kibiashara (marketing mix) kwa siku za usoni.


Kurasa zisizoweza kutambazika

Watembeleaji wa website Tanzania huwa wanascan
Tumewahi kuandika sana, na tutaendelea kuandika, watembeleaji wa website kipindi wanatafuta makala / taarifa huwa hawasomi, bali wanatambaza (scan), na wengi wa watembeleaji hawa huondoka pindi wanaposhindwa kupata matokeo waliyoyategemea.
Wengi wa wamiliki wa website wa Tanzania, wanaangukia hapa. Wamiliki wengi wanashindwa kutoa picha ya website yao kwa jicho la kwanza. Website na Blog nyingi za Tanzania zimejaa sana, yaani mtembeleaji anashindwa hata pa kuanzia. Hautakiwi kuandika maneno milioni moja ili kumfanya mtu atumie website yako kwani hatembeleaji hawa hawana muda wa kuanza kudokoa kitu kimoja kimoja.
Hili kuweza kukabiliana na tatizo hili, hakikisha uunakuwa na mpango kabla ya kuanza ujenzi wa website, pia tumia muda wako kushauriana na kampuni inayokutengenezea website yako ili kuhakikisha wanapata maana halisi ya kampuni yako. Bila kusahau, jaribu kujua tabia za online za Watanzania (Online behaviors).

Changamoto kubwa ambayo tumekuwa tukikutana nayo Dudumizi ni kitendo cha wafanyabiashara wengi ni kutaka kuhamisha kila kilicho offline kukipeleka online, yaanni wengi wanadhani, kuwa na makala mengi ndio kushinda kwao. Hivyo hutulazimu kutumia muda mwingi kuwaelekeza juu ya jinsi gani wanaweza kuandaa makala nzuri na zenye kushiba.

Kukiacha Kiswahili

Matumizi wa kiswahili kwenye Website Design TanzaniaKiswahili kikiwa lugha ya Taifa inayoongewa na asilimia kubwa ya Watanzania, lakini, leo hii utakuwa wamiliki wengi wa website wanatumia Kingereza kwenye kila sehemu huku wateja wao wakubwa wakiwa ni wazungumzaji wa kiswahili. Matumizi ya kingereza, sio tu huwafanya watu wakuone KAMA wale ikimaanisha kutokuwa na utofauti, pia huondoa ile hali ya kuwafanya wajione wapo nyumbanii, kwa mfano, binafsi, ni kitu kilichotokea bila mwenyewe kujua,siwezi kusoma habari za Tanzania kwenye website yoyote ya kingereza, na nikisoma basi nitalala au kuachana nayo na kufanya mambo mengine, na hii pia ni vilevile, nikitaka kusoma habari za China, huwa ninasoma kwa Kichina, vilevile hutumia kingereza kuangalia au kusoma habari za dunia. Hivyo kwenye ubongo wangu nimeshaufanya ufuate mtindo huo. 

Pia,kuna maelfu ya watembeleaji ambao wangehitaji huduma yako, lakini kwakuwa ipo kwa kingereza wateja hawa hawatokuwa wa kwako, kwakuwa kuna website nyingi sana toka marekani na UK zilizoanza miaka kibaoo nyuma zinatoa huduma kama wewe, hivyo hapa wewe kiswahili ni moja ya nuru yako, pia jiandae kwa kesho ambapo Kiswahili kitakuwa ni moja ya lugha zinazotumia sana kwa Afrika pia kwa kuwa  na makala za kiswahili, kutakusaidia kupunguza mashindano kwenye mitandao utafutaji (search Engines).
Hivyo, kabla ya kuamua unatumia lugha gani, unatakiwa kusoma na kunyanyambua takwimu kujua idadi ya watembeleaji wako kama nilivyoelezea hapo juu, pia kujua muelekeo wa biashara yako, nani mteja wako (marketing segment), baada ya hapo ni dhahiri utaweza kufanya maamuzi yenye kujenga biashara yako. Pia, ikumbukwe kuwa, unaweza kutumia lugha zaidi ya moja, AWM tukiwa na wateja wengi toka nchi mbalimbali duniani, hivyo, suala la lugha ni moja ya kitu ambacho tumekuwa tukijadiliana na wateja wetu kabla ya kuanza project yoyote. Tumekuwa tukishauliana na wateja wetu juu ya matumizi bora ya lugha.

1 comment: