Chapisho Jipya

google adsense ni nini?

Image result for what is GOOGLE ADSENSE?
Mimi ni mtumiaji wa google adsense kwa kipindi cha miaka 4 iliyopita 
au zaidi , kupitia adsense nimeweza kupata kipato cha kuendesha maisha 
yangu kwa njia mbalimbali , kama ujenzi wa nyumba na uendeshaji wa 
biashara nyingine kupitia kipato hicho tu . 

Watu wengi wanapenda kujiunga na adsense na wengine walijiunga 
wakakata tamaa au hata wengine akaunti zao kufungiwa kutokana na 
kukiuka masharti kadhaa ya google adsense , mimi mwenyewe nilifungiwa 
mara 3 hivi na nilipoteza zaidi ya milioni 5 za kitanzania . 

Hili ni somo fupi kwa wale wanaopenda kujiunga na adsense au ambao 
wameshajiunga lakini wanataka kupata faida zaidi . 

Google Adsense ni nini ? 
Google adsense ni mfumo wa matangazo wa Google ambao unamwezesha mtu 
kitangaza bidhaa zake kwa kipato alichotacho na kumwezesha mwenye 
tovuti au blogu kufaidika kutokana na matangazo ya adsense kuonekana 
kwenye blogu yake au tovuti yake . 

Kwa lugha rahisi tunaweza kuita ppc Pay Per Click , Lipa kwa Click au 
mguso mmoja kwenye tangazo husika , mimi mwenye blogu hela utakuja 
kwangu kama mtu aligusa au gonga tangazo alilioona kwenye blogu yangu 
na yule aliyetangaza bidhaa zake kwenye google hela ndio inakatwa 
kutokana na click hiyo . 

Mimi nina blogu nyingi ambazo nimejisajili na google adsense , 
ukiingia kwenye blogu hizo utaona matangazo yanaonekana yale matangazo 
sijaweka mimi na sijuani na walioweka matangazo hayo mimi yangu ni 
blogu na nafasi ya kutangaza niliyoiweka kwenye blogu . 

Unajiungaje na Adsense ? 

Adsense ni mali ya Google ni lazima au vizuri uwe na barua pepe ya 
gmail ambayo ni ya google au nyingine ambayo itakuwezesha kuweza 
kusajili adsense kwa urahisi lakini ni vizuri iwe imesajiliwa google . 

Usajili unakuwaje ? 

Tembelea www.google.com/adsense ukishasajili inachukuwa siku 15 kwa 
tovuti yako au blogu yako kuangaliwa kama inakidhi viwango vya google 
adsense kama lugha ,picha ,maudhui ,rangi na copyrights . 

Unaposajili unapewa CODE maalumu ambazo unaweza kuweka kwenye kurasa 
za tovuti au blogu yako kwa ajili ya kuanza kuonyesha matangazo 
mbalimbali . 

Nikisema lugha nina maanisha utumie lugha zinazokubalika na adsense 
kama kiingereza , kifaransa na nyingine za kimataifa Kiswahili 
hakitakiwi labda uchanganye ,kama blogu au tovuti yako ina picha chafu 
haitakiwi , rangi zake ziwe nzuri zisiingilie maslahi ya matangazo ya 
adsense na angalia milki ya vile unavyoweka . 

Baada ya siku 15 inakuwaje ? 

Baada ya siku 15 utapata email kama umekubaliwa au umekataliwa kama 
imekataliwa unaweza kuangalia ulichokosea na kubalisha kwa kukata 
rufaa unatakiwa ujaze appeal form ambayo nayo itaangaliwa kwa siku 
15 . 

Kama umekubaliwa basi unatakiwa kuingiza dola 100 au euro 70 , hela 
hizi zinapatikana kutokana na matangazo yanayoonekana kwenye blogu au 
tovuti yako , ukiwa na kipato hicho utatumiwa kadi yenye namba ya siri 
ambayo utaingiza kwenye akaunti yako ili uweze kukamilisha usajili 
wako wa adsense , mlolongo huu unaweza kuchukuwa miezi 2 hivi . 

Unalipwaje ? 

Inategemea umechagua mfumo gani wa kulipwa , kuna mifumo 3 hivi 
inayojulikana zaidi . 

a)        Cheki – njia hii ilikuwa inatumika zaidi zamani hata sasa hivi kwa 
baadhi ya nchi na wale wanaopenda , kwa wale wa afrika inachukuwa siku 
7 kupata cheki yako hapo utakatwa euro 17 kwa ajili ya kusafirisha 
cheki hiyo ,halafu unatakiwa kuingiza cheki kwenye akaunti yako ya 
benki ambapo inachukuwa siku 21 kulipwa au zaidi ya hapo – benki 
nyingine hazikubali cheki hizi kwahiyo wanaweza kukataa , kama 
ikikubali benki itakata hela ya kuprocess cheki . 

b)        Uhamisho wa Benki – Njia hii pia ni nzuri lakini kuna hela Fulani 
unakatwa kwa ajili ya kuhamisha hela kutoka nchi moja kwenda nyingine 
kwa njia ya benki na sio benki zote zenye huduma hii na inategemeana 
na kiwango cha hela inayotumwa kama ni ndogo sana inaweza kuwa tabu 
kidogo . 

c)        Western union – Hii ndio bora na ya haraka zaidi mara nyingi 
inalipwa kila mwisho wa mwezi unaofuatia kama ulipata dola 600 mwezi 
wa 3 utalipwa mwezi wa 4 mwishoni baada ya mahesabu kukamilika na 
baada ya kukatwa kodi na masuala mengine muhimu . 

NINI KISICHOTAKIWA ? 

1 – Huduma nyingine za Matangazo , Kwa sababu adsense ni Pay Per Click 
ni bora usiweke matangazo mengine ya PPC kwa sababu yataingiliana na 
maslahi ya adsense unaweza kufungiwa au kuweka huduma nyingine za 
matangazo ambazo zinaweza kuzorotesha huduma za matangazo ya adsense . 

2 – Kulazimisha watu kugonga au click au wewe mwenyewe kufanya hivyo , 
hutakiwi kulazimisha watu kugonga matangazo ili ujiongezee 
kipato ,waache waangalie na kuamua wenyewe , kazi yako iwe ni kuweka 
taarifa za kutosha kwenye blogu au tovuti yako zinazovutia watu 
kutembelea na kuvutia watu wa masoko kupitisha matangazo yao kwenye 
kurasa zako . 
Hiyo namba moja ndio ya kwanza na muhimu zaidi nyingine ni Lugha , 
haki miliki , picha chafu na rangi nzuri kwenye kurasa zako ambazo 
zitafanya matangazo kuonekana vizuri . 

FAIDA KWA MWENYE BLOGU TOVUTI 
Kutegemeana na aina ya blogu yako na maudhui lakini blogu au tovuti 
ili iweze kupata zaidi ya dola 15 kwa siku inatakiwa angalau kuwa na 
watembeleaji wa siku moja zaidi ya alfu 3000 , wanaotembelea toka nchi 
zinazoendelea na kuclick toka nchi za ulaya ndio wenye fedha na 
kuwezesha kulipwa vizuri zaidi kuliko nchi za afrika . 

Kwa Tanzania blogu ya kawaida yenye watembeleaji kati ya 2000 au 4000 
kwa Tanzania inatakiwa iwe na shilingi laki 9 kwa mwezi mmoja au zaidi 
kama kipato chake 

FAIDA KWA WATANGAZAJI /WAFANYABIASHARA. 
Utangazaji kwa kupitia adsense ni rahisi na fedha yako inaenda 
kihalali na ni rahisi kutokana na bajeti yako kama umepanga kutangaza 
kwa laki 1 kwa mwezi na unataka tangazo lako lionekane Tanzania pekee 
basi kwa kupitia adsense hiyo inawezekana kama unataka lionekana kwa 
lugha ya kiingereza pekee na lionekane japan au korea hilo 
linawezekana ni wewe kuamua na kufanikisha hilo kupitia adsense . 

Kama wewe ni mfanyabiashara huhitaji kuhangaika kutafuta blogu au 
tovuti kubwa kutangaza bidhaa zako ambako inaweza kuwa gharama zaidi 
na kupata nafasi ni finyu , fikiria adsense ifanyie kazi . 

ADSENSE INAWEZA KUWA AJIRA TOSHA ? 
Inategemea na mipango yako lakini adsense sio ya kuitegemea sana kama 
usipofuata taratibu unaweza kufungiwa lakini kama ukifuata masharti na 
kukaa nayo vizuri inaweza kuwa ajira yako inayokulipa vizuri na 
kufanya maisha yako kwenda vizuri . 

ADSENSE SIKU ZIJAZO . 
Sasa hivi watu wanatumia simu za mikononi na vifaa vingine kwa ajili 
ya kutembelea tovuti na blogu sio komputa kama zamani , kama ni 
mtumiaji wa adsense jiandae kwa hilo hakikisha matangazo yako ni 
mepesi na yanaweza kuonekana au kusomeka na watu wanaotuvmia vifaa 
hivi na kukulipa vizuri bila usumbufu mwingine . 

Kama unapenda kujua zaidi kuhusu adsense na msaada zaidi unaweza andika barua pepe au comment hapo chini kama sipatikani andika sms kama uko Dar es 
salaam au Nairobi au Juba ni rahisi kuonana tunaweza kusaidiana .
chanzo 

Yona F Maro 

6 comments:

  1. leo ndo nimeelewa zaidi ahsante kwa somo zuri

    ReplyDelete
  2. Asante naweza kupata nambayako

    ReplyDelete
    Replies
    1. hello ssein, naomba niandikie namba yako ya wasap hapa kwani kwa sasa sipo nchini kwa hiyo namba ya kawaida haitasaidia sana

      Delete
  3. Je mkuu nawezajee kufungua blogger ..
    Pia naruhusiwa kutumia Card bank yeyote ya bank kama ni CRDB nikapata mkwanja

    ReplyDelete
    Replies
    1. ndiyo inaweza kufanya kazi .na kuhusu kufungua blogger wana chapisho lisome

      Delete
  4. Habari ya uzima ndg: kwanza nashukuru sana kwa taarifa yako hii ya namna ya kunufaika na google adsense, mimi naomba msaada juu ya mambo haya,
    1) Je kunauwezekano wa kuitengeneza blog mwenyewe hata kama sina ujuzi juu ya maswala ya computer?
    2) Je baada ya kufungua blog ninawezaje kuiunganisha google adsense na blog yangu tayari kwa malipo?
    naomba msaada zaidi, +255655119632 whatsap

    ReplyDelete