NJIA HIZI 5 ZITAKUINGIZIA KIPATO UKIWA INTERNET
Bila shaka unapata manufaa kadha wa kadha kupitia internet. Je, unaingiza fedha kupitia mtandao, au wewe ni mtu wa kutumia tuu fedha kwa ajili ya internet lakini bado haujaanza kuingiza fedha kupitia mtandao? Makala hii inachambua namna ambavyo unaweza kutumia internet kuingiza kipato.
1.Kutafutia watu taarifa: Wapo watu wengi wenye shida ya kupata taarifa fulani kwa uharaka na kwa usahihi, hata hivyo wanakumbwa na vikwazo vingi kama vile wapo ‘bize’ sana –hata kama wanayo kompyuta na internet connection masaa 24, au pengine ni kwakuwa hawana ujuzi wa kutosha wa kupata taarifa kwa ufanisi zaidi. Watu wa aina hii pengine ni wanafunzi wa elimu ya juu, wafanyabiashara au watafiti wa fani mbalimbali. Uwezo wako wa kutafuta taarifa kwa ufanisi, na kuweza pia kutambua wateja walengwa wa huduma hii , kunaweza kukufanya kuingiza kipato.
2.Kuuza bidhaa kwa bei poa kabisa: Kupitia internet utaweza kupata taarifa za bei za bidhaa mbalimbali. Umakini na juhudi zako za kutafuta bei nafuu zaidi kunaweza kukufanya ukajua bei poa kabisa za bidhaa fulani, kasha ukatafuta wateja wa kuwauzia bidhaa hizo. Jambo hili limerahisishwa sana siku hizi kwa kutumia mitandao ya kijamii kwani wapo watu tayari ambao huingia kwa mitandao ya kijamii kama Facebook, wakitaja aina ya bidhaa wanazotafuta. Tembelea pata pesa mtandaoni group la Facebook, utajiona fursa hii.
3.Kutangaza bidhaa za watu/makampuni: Kupitia mtandao mkubwa utakaoweza kujenga kwa kutumia internet, utaweza kutangaza bidhaa za watu au asasi mbalimbali. Mfano waweza tangaza bidhaa za watu kupitia blogu yako(yenye wasomaji wengi), au kupitia ukurasa wako wa Facebook, au kupitia huduma maalum ya kutangaza kwa barua pepe, ambapo utawaomba watu wajiandikishe kupata updates mbalimbali ikiwemo matangazo ya ofa mbalimbali za bidhaa. Waweza pia tangaza bidhaa kwa website/blogu yako kwa kupitia Affiliate programs, ambapo utalipwa kuendana na ‘clicks’ zitakazoingiza wateja kwa asasi fulani.mfano wa affiliate ni kama adiboye na kadhalika
4.Kutangaza bidhaa zako: Kuna njia nyingi za kutangaza bidhaa zako kupitia internet, kuanzia kutangaza bure au hata kulipia matangazo yako. Waweza kutumia akaunti yako ya Facebook au GooglePlus kutangaza bidhaa zako. Waweza tengeneza blogu na kupitia blogu hiyo ukaweka matangazo yako. Au ukaamua kulipia matangazo kwa blogu za watu wengine, ukatangaza kupitia Facebook, na website mbalimbali.
5.Kuandaa kipato kikubwa cha baadae: Ukiachilia kupata kipato cha haraka haraka kwa wakati huu, unaweza kutumia mtandao kuandaa mapato makubwa ya baadae. Unaweza kufanya hivi kwa kutumia internet kujenga mtandao utakaokusaidia hapo baadae-mfano kutumia Linkedin, Facebook au Twitter kujenga mahusiano na watu ambao baadae watakuwa wateja wa bidhaa zako, au washirika katika biashara, au hata waajiri wako wa baadae. Pia waweza kutumia internet kujenga ufahamu na ujuzi fulani ambao hapo baadae utaweza tumia ujuzi huo kuingiza kipato. Mfano kuna website nyingi zinazotoa mafunzo bure ya ujuzi adimu kama website design, programming, marketing, n.k.
Hitimisho
Ukitafakari maelezo hapo juu , utaona kuwa kuna mianya mingi ya jinsi ya kuingiza kipato kwa kupitia internet. La msingi ni matumizi yako ya busara ya internet, na kuendelea kujifunza siku hadi siku namna bora ya kuboresha matumizi yako ya internet. Hata kama kwa sasa unadhani unaingiza kipato cha kutosha, hautodhurika kwa kujifunza njia nyingine za kuongeza kipato chako.
No comments