MADA ZITAZOWEZA KUKULETEA WATEMBELEAJI WENGI KATIKA BLOG AU WEBSITE YAKO
Kutokana na mfumo wa maisha ya mwanadamu kila mtu hupendelea vitu fulani ambavyo si lazima vifanane na vya mtu mwingine.Japo yawezekana kuna baadhi ya mambo hupendwa na wengi na hayo ndiyo mambo ambayo sisi tutayazungumzia hapa.Hayo mambo ndiyo yatakufanya wewe upate watembeleaji wengi kwa tovuti yako.
kwa namna nyingine watembeleaji ndio husaidia pia kukuongezea kipato chako cha matangazo mfano adsense
- kama hujajiunga na adsense angalia vitu vya muhimu kabla ya kujiunga hapa
MAMBO HAYO NI KAMA YAFUATAYO;
1.UDAKU NA HABARI MOTOMOTO
Hii kwa nchi nyingi imekuwa ni chanzo kikubwa cha watu kujipatia mamia ya maelfu ya watembeleaji kwani watu wengi wanapendelea mambo ya kupata habari kemkem za kiutafiti ambazo pengine huwa ni vitu vidogo visivyo na msingi lakini hapo ndipo watui wengi hupendelea.
2.BURUDANI NA MICHEZO
Watu wengi pia hupenda kupoteza mda mwingi mtandaoni wakizungukia tovuti za burudani na michezo kwani watu hupenda sana kufuatilia michezo ile waipendayo hivyo ukiandika blog ya burudani na michezo unaweza jipatia wwatembeleaji wengi sana.
3.USHAURI WA KITAALAM
Hizi ni tovuti za namna yake ambazo ,mara nyingi huwa na mada fulani mfano AFYA,UFUNDI,MASOMO na kadhalika ambazo huwa zinaelezea mada yake na kutoa ushauri wa kitaalamu.hizi pia hupendwa sana na watu. mfano wa tovuti hizo ni afya zetu 360 bofya uone mfano huu
4.MITINDO
Tovuti kama hizi za mitindo huwavutia zaidi watembeleaji wakaao mjini hasa wale vijana zaidi kwani wao ndio mda mwingi hujihusisha na mitindo hii hufanya pia watu wapate watembeleaji katika tovuti zao.
5.MATANGAZO
Kuna tovuti za namna nyingine ambazo ni tovuti za matangazo yaani watu wanaweka matangazo yao ya mauzo katika tovuti fulani.Tovuti hizi huwa na watembeleaji wengi kuliko kawaida kwani anaeweka bidhaa na anaeenda ku nunua wote huingia katika tovuti husika hivyo watembeleaji huwa ni wengi mno tovuti ikijulikana.mfano ni kupatana bofya uone mfano wake
Hizo ni baadhi tu ya mada japo zipo nyinginezo
Hizo ni baadhi tu ya mada japo zipo nyinginezo
No comments